Project Details

Posted On : 23-08-2019

Miradi ya Kuendeleza Makao Makuu Dodoma

Project Description

Serikali ya awamu ya tano (5) chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ilitangaza rasmi mpango wa Serikali kuhamia makao Makuu Dodoma Julai 25 2016 wakati wa maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa nchini ambayo kitaifa yalifanyika katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa Mkoani Dodoma.

Location Tanzania
  • Key Figures

  • Employees
    0
  • Status
    Starts

Lengo kuu ikiwa ni kutimiza ahadi ya Rais wa awamu ya kwanza, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoitoa mwaka 1973 ya kulifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi. Rais alisema “Nataka yote tuliyoyaahidi tuyatekeleze, Alisisitiza, “ jukumu langu lilikuwa kutekeleza ahadi ya Mwalimu Nyerere, na nilipata nguvu baada ya kukumbuka kuwa ziko nchi nyingi tu duniani ikiwemo nchi za Afrika kama Nigeria na Cote d’Ivoire ambazo zilihamisha makao makuu ya nchi yao katika kipindi kifupi.

Mji wa Dodoma ambao umetangazwa rasmi kuwa Makao Makuu ya Nchi

wananchi, pamoja na kusaidia ukuaji wa uchumi katika mikoa iliyopo katikati ya nchi.

Miradi na fursa za Serikali kuhamia Makao Makuu:-

1.Miradi

    • Ujenzi wa Majengo ya Mji wa wa Serikali,
    • Ujenzi wa Uwanja Mkubwa wa Michezo,
    • Ujenzi wa barabara itakayogharimu bilioni 500 kwa mkopo wa fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itakayojengwa kutokea Mtumba, Veyula na Nala ambayo ina urefu wa kilomita 4,
    • Ujenzi wa uwanja wa ndege mkubwa na wa kimataifa unaogharimu bilioni 400,
    • Maandalizi ya ujenzi wa Bandari kavu kwa vile jiji la Dodoma lina kituo kikuu cha reli ya kisasa (SGR),
    • Kituo cha afya katika mji wa Serikali kitakachogharimu bilioni 4.5.
    • Ujenzi wa shule ya sekondari ya kisasa itakayogharimu shilingi bilioni 13 na Chuo cha mafuzo (VETA) kitakachogharimu shilingi bilioni 18. Ikiwa ni pamoja na kuendelea kuimarisha hospitali ya Benjamini Mkapa ambayo imeanza kutoa matibabu ya kibingwa.

2. Fursa

    • Mafundi wa aina mbalimbali,
    • Vibarua,
    • Kuongezeka kwa mahitaji mbalimbali za kibinadamu kama vile vyakula, maji, dawa, n.k;
    • Mahitaji ya vifaa vya ujenzi,
    • Shule na vituo vya afya,
    • Migahawa, nyumba za kulala wageni, Mahoteli n.k,
    • Usafiri wa aina zote,
    • N.K.

3. Mafanikio

Tangu Serikali itangaze rasmi mpango wa kuhamia mkoani Dodoma, mambo yafuatayo yamefanyika;-

    • Wizara na idara mbalimbali za Serikali zimeshahamia Dodoma,
    • Zaidi ya watumishi 3,800 wameshahamia Dodoma hadi kufikia April 2018,
    • Ofisi ya Waziri mkuu imeahamia Dodoma,
    • Ofisi ya Makamu wa Rais imehamia Dodoma,
    • Uzalishaji umeme megawati 48 umekamilika, huku mahitaji halisi yakiwa megawati 28,
    • Ujenzi wa barabara za mzunguko ndani ya Dodoma yenye urefu wa kilomita 39 umefikia hatua nzuri,
    • Ujenzi wa awali wa Mji wa serikali umekamilika na kuzinduliwa na Mh Rais,
    • Kupandishwa hadhi Manispaa ya Mji wa Dodoma na kuwa Jiji, Aprili 26, 2018,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli akizindua rasmi mji wa Serikali uliopo katika kata ya Mtumba jijini Dodoma.

Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akionesha hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa tenki la maji ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali.