Bandari

BANDARI

Bandari ya Mtwara

Hatua iliyofikiwa

katika kazi zilizopangwa za ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 300 kuboresha mfumo wa usalama wa meli na kukarabati gati Na. 3 na la Lindi ni: kukamilika kwa asilimia 20 ya ujenzi wa gati moja (multipurpose terminal) lenye urefu wa mita 300.

Bandari ya Tanga

Hatua iliyofikiwa

kuendelea na kazi ya kufanya upembuzi yakinifu wa kuboresha bandari, ujenzi wa gati Na. 2 na barabara ya kuingia katika gati namba 2. Kwa upande wa ujenzi wa gati la Chongeleani, hatua iliyofikiwa ni kufikia hatua ya mwisho ya majadiliano ya kuendeleza ujenzi wa gati hili kati ya mkandarasi wa ujenzi na Serikali mbili za Tanzania na Uganda.

Bandari ya Dar es Salaam:

hatua iliyofikiwa ni:

Kusainiwa kwa mkataba wa utekelezaji wa mradi; kukamilika kwa ujenzi wa makazi ya wahandisi, maabara ya ujenzi na kuwasili kwa mashine za ujenzi; kuendelea usanifu wa Gati Na. 1 - 3; na kuanza ujenzi wa gati la kuhudumia meli za magari (RoRo berth) kwa kujaza kifusi katika eneo la mradi la Gerezani Creek.