Fedha

Mradi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara Tanzania (TFED) (1993 - 1997) ulisaidia Serikali ya Tanzania kuweka mfumo wa mageuzi na hatimaye ukombozi wa sekta ya fedha. Kabla ya mwaka 1995, benki za umma zilitawala soko. Viwango vya riba vilikuwa juu sana, uwekezaji ulifanywa bila kufuata misingi ya ukuaji wa kiuchumi / kifedha, gharama ya kukopa ilikuwa kubwa sana pia huduma ya kukopesha katika sekta binafsi ilikuwa kwa bidhaa ndogo ndogo na kwa mkopo wa muda mfupi.

Mabadiliko yaliyotolea katika sekta ya fedha yaliwezesha benki za umma na serikali kuingia katika soko huria. Viwango vya riba za vilitegemea viwango vya soko kwa muda huo, benki ambazo zilishindwa kuendana na kasi ya soko la fedha ama zilifungwa au kufanyiwa marekebisho huku zingine zikiuzwa na zaidi ya hapo benki zote mpya za ndani na benki za kimataifa ziliingia sokoni. Orodha ya benki zinazofanya kazi nchini Tanzania ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini.

a) Benki za Kigeni

  1. Citibank (USA)
  2. Benki ya Barclays (UK)
  3. Benki ya Standard Chartered (SA)
  4. Amalgamated Bank of South Africa – bought National Bank of Commerce
  5. Stanbic Bank (South Africa)
  6. Benki ya Biashara ya Kenya
  7. Benki ya Malaysia
  8. Benki ya Habib (Pakistan)
  9. Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki
  10. United Bank of Africa
  11. Benki ya Euro Africa

b) Benki za Ndani

  1. Benki ya CRDB
  2. Benki ya Biashara ya Akiba
  3. Tanzania Investment Bank
  4. AZANIA Bankcorp
  5. National Micro Finance Bank
  6. CF Bank
  7. EXIM (T) Bank
  8. National Bureau de Change
  9. Benki ya Posta
  10. Kilimanjaro Cooperative Bank na
  11. Small Community Banks in Dar es Salaam,
  12. Mwanga, Njombe and Mufindi

c)Taasisi zingine za kifedha

  1. Tanzania Development and Finance Limited
  2. Capital Finance Ltd.
  3. Fedha Fund Ltd
  4. Savings and Finance Ltd

d)Taasisi zisizo za kifedha zinazotoa huduma za kifedha

  1. Social Action Trust Fund (SATF) – Seed fund of $ 10 million given by USAID to lend to large enterprises in private sector
  2. Risk Management and Profit Sharing Fund (RMPS) – Seed Fund of $ 2 million given by USAID to lend to Small and Medium Enterprises
  3. Mtaji Fund – Seed fund of $600,000 given by SNV – Netherlands
  4. Small Enterprise Loans Fund (SELF) – Seed Fund of $8 million loaned to government from ADF for lending to Micro Finance Institutions and about 12 NGOs that are donor funded. There are also Credit Reference Bureaus to offer information related to credit in the Banks and financial institutions.
Fursa zinazopatikana kwa ajili ya sekta hii zinahusiana sana na wawekezaji makini na pia kutoa huduma kwa idadi kubwa ya benki za jamii ambazo zinahitaji teknolojia ya utoaji wa huduma bora. vikwazo kwa ukuaji wa mabenki ya biashara ni uhamasishaji wa kuweka akiba kwani benki nyingi bado hazijaweza kufikia wafanya biashara wadogo katika soko la vijijini. Kwa sasa mtandao wa mabenki ya biashara umeenea zaidi kwenye maeneo ya mijini mikubwa na miji midogo au pembezoni mwa maeneo hayo . Ukosefu wa benki ya maendeleo umekuwa kikwako kikukwa ambacho kinarudisha nyuma mchango wa secta ya fedha katika ukuaji wa uchumi na sekta zingine kama kilimo, viwanda, utalii n.k, sekta hizi zinahitaji mkopo wa muda mrefu ambapo kusema kweli hautolewi na benki hizi.


Kuna haja ya kuboresha mazingira na mfumo wa kisheria na mahakama ili kuongeza ushiriki wa ndani katika sekta za fedha. Mfumo kama huo unafaaa kutumika zaidi katika kuondoa changamoto katika sekta ambazo bado ni changa na pale ambapo kuna upatikanaji mdogo wa huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wadogo na elimu duni ya kifedha kutokana na wafanya biashara wadogo kujikita katika shughuri zinazo wapatia kipato cha kujikimu tu, changamoto za miundo mbinu hasa barabara na majengo bado itaendelea kuwa kikwazo kikubwa kwa watanzania wengi wenye kipato cha chini waishio vijijijni.

Kiwango cha mitandao ya kibenki kuanzishwa vijijini ni mdogo kwa asilimia nane (8) katika Tanzania bara, kimsingi inasabaishwa na mazoea ya benki nyingi kupenda kutoa huduma katika maeneo ya watu wengi na kwa maeneo yenye shughuli nyingi za kuchumi.