Ajira

Uwepo wa wafanyakazi wenye ujuzi ni jambo la msingi katika kuwezesha nchi kufikia kipato cha kati ifikapo 2025.Wafanyikazi wengi nchini Tanzania wana kiwango cha chini cha ujuzi ambapo asilimia 79.9 ya walioajiriwa wako kwenye kiwango cha chini, Asilimia 16.6 wako kwenye kiwango cha kati, na asilimia 3.6 tu wako kwenye kiwango cha juu cha ujuzi. Hatua za makusudi hazinabudi kuchuliwa ili kujenga ujuzi wa watanzania katika sekta za kipaumbele kwa kuhakikisha kuwa wawekezaji wanaweka mipango mahususi ya ajira ambayo itaonyesha wazi mipango ya kuwajengea uwezo wafanyakazi, mpango wa urithishaji madaraka na ufuatiliaji madhubuti unafanywa ili kuhakikisha watanzania sio tu wanaajiriwa katika kazi zisizo na ujuzi lakini pia katika kazi nyingi za kitaalam na manejimenti