Bima

Sekta ya bima nchini Tanzania inasimamiwa na Sheria ya Bima ya mwaka 2009 (kama ilivyorekebishwa). Sekta hii ina jukumu muhimu ndani ya uchumi wa taifa kwa kutoa uwezo wa kuthibiti vihatarishi na kuchangia uhamasishaji wa kuweka akiba kwa maendeleo endelevu ya uchumi wa nchi. Sekta ya bima inawezesha uchumi kufanya kazi kwa ufanisi. Bila kuwepo kwa utaratibu madhubuti wa kuaminika wa kuzuia au kuondoa vihatarishi, shughuli nyingi za kiuchumi zingekuwa kwenye mazingira hatarishi. Kwa hivyo juhudi za kuboresha utendaji wa uchumi na viwango vya maisha vya watu lazima zizingatie maendeleo ya sekta ya bima. Tarifa ya TIRA ya mwezi Septemba 2016 imeeleza kuwa, biashara ya bima ilikua kwa asilimia 11.76% ya mapato ya jumla kutoka TZS 410,741 milioni katika kipindi kilichoisha Septemba 2015 hadi milioni 459,036 milioni katika kipindi kilichoisha Septemba 2016.

Sheria ya Bima ya mwaka 2009 kama ilivyorekebishwa imezingatia ushiriki wa watanzania katika sekta ya bima kwa kuweka wazi idadi ya hisa zitakazomilikiwa, kiasi cha mtaji au haki ya kupiga kura zinazotakiwa kushikiliwa na watanzania katika kampuni za bima na kwa madalali (brokers). Pia inaeleza kuwa bima yoyote inayotekelezwa na mtanzania au kampuni ya inayomilikiwa na mtanzania ya daraja lolote itawekwa na bima ya Mtanzania. Kulingana na ripoti za TIRA kuna kampuni 31 za leseni zilizo na leseni na madalali 124.

Licha ya kuwa na mfumo mzuri wa kisheria Sekta bado inakabiliwa na changamoto kama vile uwezo mdogo wa upimaji kushiriki katika sekta muhimu zinazojitokeza za mafuta na gesi kutokana na uwezo mdogo wa kiufundi na kifedha. Hii itasababisha uwekaji mkubwa wa bima kwa kampuni za bima za nje na hivyo kupunguza rasilimali za ufadhili ndani kwa maendeleo ya uchumi. Pia upungufu wa nidhamu muhimu za bima pamoja na sayansi ya msingi kwa sababu ya uwezo mdogo wa taasisi za mafunzo kutoa sifa zinazofikia viwango vya kimataifa. Zaidi ya hayo, mashirika mengine ya kimataifa hayaweki wazi kwamba yana bima ya nje. Baadhi ya mashirika pia yanazidisha kwa makusudi kiasi kinachochukuliwa nje ya nchi ili kuondoa uwezo wa ushiriki wa bima wa ndani.