mawasiliano

Sekta ya mawasiliano Tanzania ni sekta ambayo inaushindani wa hali ya juu, zaidi ya asilimaii 70 ya watanzania wanatumia simu za mkononi, hata hivyo kila mwaka idadi linaongezeka kwa asilimia 20 zaidi. Vita ya ushindani wa soko la bei miongoni mwa makampuni kubwa za simu zimeathiri sana kampuni nyingi ndogo ambazo zinakabiliwa na changamoto ya kuondoka kwa wateja.

Soko la mawasiliano ni la ushindani sana na makumpuni zifuatazo zinatoa huduma za mawasiliano:

Simu za mezani

  1. Tanzania Telecommunications Company Limited (TTCL)
  2. Zanzibar Telecommunications Limited (ZANTEL)

Simu za mikononi

  1. Tanzania Telecommunications Company Limited (TTCL)
  2. Zanzibar Telecommunications Limited (ZANTEL)
  3. Vodacom Tanzania Limited (Vodacom)
  4. MIC Tanzania Limited (TIGO)
  5. Airtel Tanzania Limited (Airtel)
  6. .Benson Informatics Limited (Smart)
  7. Dovetel (T) Limited (SASATEL)
  8. Smile Viettel

Kampuni za simu ambazo zinatoa huduma kwa taarifa ya mwaka 2015 katika soko la ushindani zina asilimia zifuatazo

Watumiaji wa huduma za mawasiliano kwa njia ya sauti

Tanzania ni nchi ya pili kwa soko la mawasiliano nyuma ya Kenya katika Jumuiya ya Africa Mashariki ambapo asilimia 79 ya watanzania ni watumiaji wa huduma za mawasiliano kwa njia ya sauti au simu za mkononi kwa mwaka 2015, vilevile watumiaji wa huduma ya mawasiliano kwa njia ya sauti kwa simu za mezani ilipungua kwa asilimia 22 kutoka 174,511 kwa mwaka 2010 mpaka 142,819 kwa mwaka 2015 kwa sasa makampuni yanayotoa huduma ni Airtel, Smart, Halotel, Tigo, Tanzania Telecommunication Company Limited (TTCL), Vodacom, and Zantel

Watoa huduma ya internet

Watumiaji wa mawasiliano ya internet kwa Tanzania yalifikia 17.3 milioni kwa mwaka 2015 (34 asilimia ya watu wote wa Tanzania ) ukilinganisha 5.3 milioni kwa mwaka 2011. Kiasi cha watu wanaotumia huduma za simu za bila waya zimeongezeka kwa kwa kasi ndani ya miaka mitano kuanzia mwaka 2011 mpaka 2015, kutoka 3.7 milioni mpaka 16.2 milioni ambayo ni hesabu ya asilimaia 90 ya watu wanaotumia internet. Smile ndio kampuni ya kwanza Africa na Tanzania iliyoanzisha mfumo wa internet wenye kasi ya 4G ndani ya mwaka 2013

Huduma ya mawasiliano kwa njia ya televisheni

Idadi ya watanzania wanaotumia mfumao wa mawasiliano kwa njia ya television ama satellite imeongezeka sana kutoka 152,216 kwa mwamka 2010 mpaka 1 milioni kwa mwaka 2014. Kulingana na namba ya kuuza vifaaa vya mawasiliano vya satellite kuongezeka kutoka 120,188 kwa mwaka 2010 mpaka 1 milioni kwa mwaka 2014 ambavyo vina Digital Terrestrial Television (DTT) .pia namba ya watoa huduma ya mawasiliano kwa njia ya satellite imeongezeka ni 46 kwa mwaka 2015. Tanzania ni nchi ya kwanza kuhama kutoka mawambi ya mawasiliano kwa njia ya analogia na kwenda katika mawimbi kwa njia ya kidigitali

Fursa zilizopo na ushirikishwaji wa wananchi

Uhuru katika sekta ya mawasiliano imefungua fursa mbalimbali kwa watoa huduma wapya wa mawasilano nchini kama vile watoa huduma za mawasiliano kwa njia ya simu za mkononi , huduma za mawasiliano kwa jamii, huduma za mitandao ya internet.

Hata hivyo huduma ya kifedha kwa njia ya simu za mkononi imeongezeka sasa kwani ongezeko la watu wanaonununa simu za mkononi Tanzania imeongezeka sana, usalama wa fedha za watanzania umeeongezeka sana.

  1. vAjira - ajira za kudumu na ajira za vipindi vifupi kwa wanachi walio wengi
  2. vHisa: Kwa sasa Vodacom ni kampuni peke za simu iliyofungua milango ya wateja wake na wananchi kwa ujumla kununua hisa.
  3. vImeongeza pato la taifa na kwa mtu mmoja mmoja

TIGO imeongeza urahisi kwenye sekta ya usafiri kupitia App inayoitwa TWENDE APP kwa ajili ya kurahisisha sekta ya usafirishaji