Barabara

MIRADI YA BARABARA

Mradi wa Ujenzi na uboreshaji wa Barabara ya Juu (Flyover) ya Mfugale

Mradi wa Ujenzi na uboreshaji wa Barabara ya Juu (Flyover) ya Mfugale, iliajiri Wafanyakazi 616 ambao kati yao 589 ni Watanzania na 27 ni Wageni. Mradi huo

uligharimu Jumla ya Shilingi 106 bilioni ambapo manunuzi ya bidhaa mbalimbali yalifanywa kwa kampuni 28 kati ya hizo kampuni zilizopo Tanzania ni 24, kampuni za nje ya nchi ni 3 na kampuni 1 ilikuwa ya ubia kati ya kampuni ya kitanzania na ya nje.

Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Jipya la Salender

Kwa kushirikiana na Serikali ya Korea Kusini, Serikali ya Tanzania inaendesha na kusimamia mradi wa ujenzi wa daraja jipya la salender juu katika Delta ya Msimbazi pembezoni mwa Bahari ya Hindi ambalo limepewa jina la “Tanzanite bridge”.

Daraja la Tanzanite linatarajiwa kuwa na urefu wa kilomita 6.2 zikiwemo 1.4 zitakazopita baharini na upana wa mita 20.5, njia nne za magari na njia mbili za watembea kwa miguu, hivyo litasaidia kupunguza msongamano wa magari kwani litakuwa na uwezo wa kupitisha tani 180 na magari yasiyopungua 50,000 kwa siku.

Ujenzi huu wa daraja la Tanzanite ambao bajeti yake ni dola za kimarekani Milioni 112.8 sawa na Billioni 258.3 za Kitanzania umefikia asilimia 50 na unatarajiwa kuwa tayari ifikapo mwezi wa 10 mwaka 2021, huku jumla ya Watanzania wapatao 402 wamepata ajira katika ujenzi wa daraja hili.

Mradi wa Ujenzi wa Barabara za Juu Ubungo (Ubungo Interchange Flyover)

Mradi huu ambao bado upo katika hatua za maendelezo lakini umetoa ajira kwa watanzania 449 (kati ya hizo, nafasi zilizohitaji ujuzi wa juu (skilled) ni 26, ujuzi wa kati (semi skilled) ni 186, na ujuzi wa chini (unskilled) ni 237) wakati idadi ya wageni ni 53 (wenye ujuzi wa Juu ni 30 na Ujuzi wa Kati ni 23). Katika manunuzi ya bidhaa na huduma 8 zilizofanyika katika hatua hii, Kampuni 7 za Kitanzania zilitoa huduma na bidhaa dhidi ya Kampuni 1 ya Kigeni.

Ujenzi wa barabara za Mwendokasi

Awamu ya pili Ujenzi huu umeanza Julai 2019 ambao unahusisha barabara za Kilwa, Sokoine, Generezani, Bandari na Chang’ombe zenye urefu wa kilometa 20.3.

Kwa sasa hivi uko katika hatua za awali.

Awamu ya tatu utakahusisha barabara za Nyerenyere, Uhuru, Bib Titi, Azikiwe ,Shauri moyo na Lindi zenye urefu wa kilometa 23.6.

Awamu ya nne utakaohusisha barabara za Sam Nujoma, Bagamoyo na Ali Hassan Mwinyi zenye urefu wa kilometa 25.9.

Ujenzi wa Barabara zingine za mikoani

Barabara ya Itoni – Mkiu – Ludewa – Manda (km 211):

Hatua iliyofikia: ujenzi wa kiwango cha lami na zege sehemu ya Lusitu – Mawengi (km 50).

Barabara ya Manyoni – Itigi - Tabora (km 259.7):

Hatua iliyofikia: hatua iliyofikiwa ni kukamilisha ujenzi wa sehemu ya Tabora – Nyahua (km 85) na Manyoni - Itigi - Chaya (km 89.3) na kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Nyahua – Chaya (km 85.4).

Barabara ya Mbeya – Makongolosi – Rungwa – Itigi – Mkiwa (km 528):

Hatua iliyofikiwa ni: kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi kwa kiwango cha lami kwa upande wa sehemu ya Chunya - Makongolosi (km 43) na kuendelea na taratibu za kupata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango lami sehemu ya Mkiwa – Itigi – Noranga (km 56.9).

Barabara ya Masasi - Songea – Mbambabay (km 659.7):

Hatua iliyofikiwa ni: kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa sehemu ya Mbinga - Mbambabay (km 66) na kuendelea na maandalizi ya ujenzi; kufikia asilimia 16 ya ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu Mtwara – Mnivata (km 50); kukamilika kwa kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara ya Masasi - Nachingwea – Nanganga (km 91.0).

Ifakara – Lupiro - Mahenge/ Malinyi – Londo - Lumecha/ Songea (km 396):

Hatua iliyofikiwa ni kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa sehemu ya Kidatu - Ifakara (km 66.9)nadaraja la Ruaha Mkuu ambapo kazi za ujenzi kwa kiwango cha lami zinaedelea.

Barabara ya Makutano – Natta – Mugumu – Loliondo (km 239) na Loliondo - Mto wa Mbu (km 213):

Hatua iliyofikiwa ni: kufikia asilimia 54 ya ujenzi sehemu ya Makutano-Sanzate (km 50), kuendelea na maandalizi ya ujenzi sehemu ya Waso-Sale (km 49); na kuendelea na taratibu za kurudia kutangaza zabuni sehemu ya Natta - Mugumu (km 41.6)


Linki ya tovuti ya miradi ya barabara: www.tanroads.go.tz