Utalii

Maliasili na Misitu

Utalii unachangia kipato cha nchi kwa mara tatu zaidi ya kilimo. Hivi sasa, ni sekta inayoongoza kwa kuchangia kipato cha nchi – ikiingiza $1bn! Kwa kuwa kuna hoteli nyingi Tanzania bara na Zanzibar za kifahari, pamoja na huduma nzuri na amani nchini, haishangazi sana kwamba Tanzania imekuwa nchi inayovutia sana.

Miradi Mikubwa ya Utalii

Mradi wa kuanzisha hifadhi ndogondogo za Wanyamapori

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amerejesha wanyamapori katika bustani za Ikulu Jijini Dar es Salaam. Ikulu sasa inapendeza.Awali wanyamapori hao walifugwa kwa idadi kubwa na Baba wa Taifa Hyari Mwl. Julius Kambarage Nyerere lakini baadaye walitoweka.
  • pamoja na hilo pia amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya kuanzisha hifadhi ndogondogo ili kuweza kujiongezea kipato. hii ni moja ya mikakati maalumu kabisa ya kukuza utalii Tanzania.

Mradi wa Kilombero and Lower Rufiji Wetlands Ecosystem Management (KILORWEMP): hatua iliyofikiwa ni:

  • kukamilika kwa Mpango wa Usimamizi na Uvunaji wa Misitu katika eneo la mradi Wilayani Ulanga na Halmashauri ya Kilombero kuandaa na kupitisha sheria ndogondogo zinazohusu maeneo ya hifadhi za jamii (Wildlife Management Areas - WMAs - 2), uhifadhi wa misitu uliojikita kwa jamii (Community Based Forest Management - CBFM - 6), na Vikundi vinavyosimamia mialo ya uvuvi, (Beach Management units - BMUs -8), uhifadhi wa maliasili uliojikita kwa jamii (Community Based Natural Resources Management - CBNRM) na usimamizi wa misitu.

Mradi wa Kuimarisha Mtandao wa Hifadhi ya Misitu kwa Utunzaji wa Bioanuai Tanzania. Hatua iliyofikiwa ni:

  • Kukamilika kwa rasimu ya sheria mpya ya Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) na marekebisho ya sheria za Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) na kanuni za Jeshi USU, ushoroba na buffer zone;
  • Kutolewa kwa mafunzo ya jeshi USU kwa baadhi ya watumishi wa TAWA;
  • Kuimarisha doria kwa kununua vifaa mbalimbali;
  • Kuandaa michoro ya ujenzi wa malango, ofisi, nyumba za watumishi na vifaa vya huduma kwa watalii;
  • Kukamilika kwa ukarabati wa mabanda 27 ya watalii, maeneo 11 ya picnic na kambi za kulala wageni;
  • Kukamilika kwa ukarabati wa viwanja vidogo vya ndege 11; na
  • Kukamilika kwa ukarabati wa kilomita 49.3 za barabara kuu za hifadhi ya Ngorongoro.

Mradi wa Kuwezesha Jamii Katika Usimamizi Shirikishi wa Misitu na Mabadiliko ya Tabia Nchi. Hatua iliyofikiwa ni:

  • Kutolewa kwa mafunzo ya utawala bora na ushiriki wa uhifadhi wa misitu na jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa wanavijiji 294, watendaji na wenyeviti wa vijiji vya mtandao wa misitu Tanzania (MJUMITA);
  • Kukamilika kwa maandalizi ya mipango minne (4) ya usimamizi wa misitu na sheria ndogondogo; na
  • Kutolewa kwa mafunzo kwa timu ya uhakiki wa misitu.
  • Kuendelea na ujenzi wa maktaba, maabara, mabweni, ukumbi wa mihadhara na ofisi za waalimu katika chuo cha misitu Olmotonyi; na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2018/19 35 kuendelea kwa ujenzi wa maabara ya ufugaji nyuki.