Habari

Imewekwa: May, 05 2021

MRADI WA GESI ASILIA TANZANIA & KENYA

News Images

Katika kuimarisha uhusiano wa kijamii na kiuchumi kati ya Kenya na Tanzania Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu amefanya ziara ya siku mbili Nchini humo na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Uhuru Kenyatta.

Moja kati ya mambo muhimu katika ziarqa hii ni utiaji saini mradi wa ujenzi wa wa Bomba la Gesi asilia kutoka Jijini Dar es Salaam kwenda Mji wa Mombasa nchini Kenya.

Tanzania inakadiriwa kuwa na futi za ujazo trilioni za Gesi asilia katika hifadhi za Nchi kavu na Baharini inayoweza kusaidia Kenya kukidhi mahitaji ya Gesi safi kwa matumizi ya nyumbani na viwandani.

Rais Samia amesema utekelezji wa mradi huu ushaanza mara moja baada ya kutia saini makubaliano hayo hivyo kinachiofuata ni usimamizi wa utekelezaji wa mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati.

Kenya ni mdau mkubwa katika biashara na uwekezaji na inashika nafasi ya 5 katika uwekezaji Nchini Tanzania kiulimwengu na nafasi ya 1 katika Nchi za Afrika Mashariki, aliongezea Mhe. Rais

Kenya imewekeza zaidi ya Dola za kimarekani 1.7 billion katika miradi 513 ambayo imezalisha ajira kwa Watanzania wapatao 51,000.