Elimu

Vijana milioni moja nchini Tanzania wanakadiriwa kuhitimu elimu katika ngazi mbalimbali na kuingia kwenye soko la ajira kila mwaka. Inatarajiwa kwamba wengi wa vijana hawa watapata fursa za kazi katika sekta binafsi. Katika kupambana na changamoto hili Wizara ya Elimu imeandaa Mkakati wa Kitaifa wa Kuendeleza Ujuzi (2016-2021). Mkakati huo unakusudia kutayarisha vijana wenye ujuzi kwa ajili ya viwanda vyenye uelekeo wa kukuza uchumi na kutengeneza fursa za ajira nchini. Mkakati unalenga wanufaika 30,000 ambao ni pamoja na wanafunzi wa vyuo Kikuu, vyuo vya ufundi, na huduma mbadala katika sekta muhimu za kiuchumi ambazo ni pamoja na utalii, kilimo na usindikaji wa mazao ya kilimo, usafirishaji, ujenzi, habari na teknolojia ya mawasiliano na nishati. Sekta zilizolengwa ni zile sekta za kipaumbele katika mkakati huu. Programu ambazo zitalenga kutekeleza mkakati huu ni zile tu ambazo zinauwezo wa kutatua mapungufu ya ujuzi wa ufundi stadi katika sekta zilizolengwa kwa lengo la kuibua fursa za mapato, kupunguza umasikini na kujenga uchumi wa viwanda

Utafiti unapaswa kufanywa katika sekta za kipaumbele ili kubaini mapungufu ya ujuzi ili hatua za makusudi zichukuliwe kufanya vijana wengi kuajirika. Anagalizo zaidi itolewe katika mafunzo kwa vitendo na ujunzi wa kujitambua, kujisimamia na kujipangia, uboreshaji wa miundombinu, mabadiliko ya mitaala, ukuzaji wa mafunzo, mafunzo ya kuanda vijana kuajiriwa, mafunzo ya uongozi, programu za mafunzo ya ndani ili kujenga ujuzi wa wahitimu na wafanyakazi kuwawezesha kuingia katika soko la ajira.