Project Details

Imewekwa : 06-09-2019

Miradi ya Viwanja vya Ndege

Project Description

​Miradi ya Upanuzi wa Viwanja vya Ndege

Mahali Tanzania
  • Key Figures

  • Employees
    3526
  • Status
    Inayoanza

Mradi wa Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam umetoa Ajira kwa Watanzania 997 (Kati ya hizo, nafasi zilizohitaji Ujuzi wa Juu (Skilled) ni 51, Ujuzi wa Kati (Semi skilled) ni 630, na Ujuzi wa Chini (Unskilled) ni 316) wakati idadi ya Wageni ni 59 wote wakiwa na Ujuzi wa Juu.

Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Kilimanjaro:

mradi unalenga kufanya usanifu wa kina na kuanza ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege, ujenzi wa barabara ya kiungio, usimikaji wa taa za kuongozea ndege na ukarabati wa maegesho ya magari ambapo shilingi bilioni 2.5 fedha za ndani zimetengwa

Kiwanja cha Ndege Mwanza:

mradi unalenga kuanza ujenzi wa jengo jipya la abiria, kuendelea na upanuzi wa maegesho ya ndege, ujenzi wa jengo la mizigo, uzio wa kiwanja pamoja na maegesho ya ndege za mizigo, ujenzi wa jengo la kuongozea ndege, kituo cha umeme, maegesho ya magari, kusimika taa za kuongozea ndege na ujenzi wa mfumo wa kuondoa maji ya mvua kiwanjani ambapo shilingi bilioni 15.55 fedha za ndani zimetengwa.

Kiwanja cha Ndege Kigoma:

mradi unalenga ujenzi wa jengo la abiria, maegesho ya ndege, usimikaji wa taa na mitambo ya kuongozea ndege, ujenzi wa jengo la kuongozea ndege, maegesho ya magari na barabara ya kuingia na kutoka pamoja na uzio wa usalama ambapo shilingi bilioni 1.410 fedha za ndani na milioni 960.75 fedha za nje zimetengwa.

Kiwanja cha Ndege Tabora:

mradi unalenga kufanya utekelezaji wa awamu ya III ya mradi inayohusisha ujenzi wa jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege, barabara ya kuingia kiwanjani na maegesho ya magari na kulipa sehemu ya madai ya mkandarasi na mhandisi mshauri wa awamu ya II ya mradi inayohusisha ukarabati wa barabara ya pili ya kuruka na kutua ndege, ujenzi wa barabara ya kiungio pamoja na jengo la uchunguzi wa hali ya hewa ambapo shilingi bilioni 1.495 fedha za ndani na shilingi bilioni 8.89 fedha za nje zimetengwa.

Kiwanja cha Ndege Shinyanga:

mradi unalenga ujenzi wa barabara ya kutua na kuruka ndege, viungio, maegesho ya ndege, jengo la abiria, jengo la kuongezea ndege, jengo la uchunguzi wa hali ya hewa, barabara ya kuingia kiwanjani, maegesho ya magari na usimikaji wa taa na mitambo ya kuongozea ndege pamoja na kujenga uzio wa usalama ambapo shilingi bilioni 2.6 fedha za ndani na shilingi bilioni 12.6 fedha za nje zimetengwa .

Kiwanja cha Ndege Sumbawanga:

mradi unalenga kulipa fidia kwa mali zitakazoathiriwa na utekelezaji wa mradi na kuanza ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege, viungio, maegesho ya ndege, ujenzi wa jengo la abiria, ujenzi wa jengo la kuongozea ndege, jengo la uchunguzi wa hali ya hewa, barabara ya kuingia kiwanjani, maegesho ya magari na usimikaji wa taa na mitambo ya kuongozea ndege ambapo shilingi bilioni 1.44 fedha za ndani na shilingi bilioni 11 fedha za nje zimetengwa.

Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato:

Mradi unalenga kuendelea na usanifu wa kina na kuanza maandalizi ya ujenzi, kulipa fidia kwa mali zitakazoathiriwa na utekelezaji wa mradi ambapo shilingi bilioni 2.41 fedha za ndani na shilingi bilioni 3.1 fedha za nje zimetengwa.