Habari

Imewekwa: Feb, 24 2021

Rais Magufuli amezindua "KIJAZI INTERCHANGE"

News Images

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli amefanya uzinduzi wa daraja la juu la Ubungo lililopewa jina la aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi aliyefariki dunia Februari 17, 2021. Rais Mgufuli amezindua barabara hiyo leo Jumatano Februari 24, 2020 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu jijini Dar es Salaam.

Amewasili eneo hilo saa 3:50 asubuhi na kufanya uzinduzi kwa kukata utepe na baadaye alikwenda kuvuta kamba na baada ya kumaliza alishuka eneo la chini la daraja hilo na kuzindua rasmi kwa kufunua jiwe la msingi lililowekwa eneo hilo.

Kabla ya kukata utepe mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Patrick Mfugale amesema Kijazi Interchange lina urefu wa mita 700 barabara ya kutoka Buguruni kwenda Mwenge na umbali wa mita 260 kutoka Kimara kwenda Manzese na kwamba barabara za chini zina umbali wa kilomita tano.

“Nimeona tuliite Daraja hili ‘Kijazi Interchange’, na naamini mtakubaliana na mimi, Mhandisi Kijazi amefanya kazi kubwa sana kwenye Sekta ya Barabara, alikuwa hana makuu, yeye ndiye alikuwa Mkurugenzi wa Barabara nchini alipotoka yeye akaja Mfugale kisha akaja Iyombe“ alisema Rais Magufuli.