Habari

Imewekwa: Sep, 10 2020

ZIARA YA NEEC MRADI WA RELI YA KISASA - STANDARD GAUGE RAILWAY.

News Images

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC limetembelea mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge Railway) Lot 1 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro. Ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utelelezaji wa Mpango wa Dhana ya Ushiriki wa Watanzania (Local Content) katika mradi wa kimkakati wa SGR.

Ziara hii ilifanyika siku ya tarehe 16 Juni 2020, ambapo NEEC ilipata nafasi yakufanya kikao cha pamoja na ya Mkandarasi Mkuu (Yapi Markez Construction Company) na Shirika la Reli Tanzania (TRC Limited).

NEEC iliweza kubaini mambo msingi mbalimbali ambayo yamewezesha kupima na kutathmini hali halisi ya utekelezaji wa mpango wa Local Content katika mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR).

Katibu Mtendaji wa NEEC Bi. Beng’i Issa amesema kwa kawaida Baraza linapokea taarifa mara kwa mara kutoka wenye miradi ya kimkakati na uwekezaji nchini, hivyo lengo la kutembelea mradi huo ni kujionea utekelezaji wa programu ya ushiriki wa Watanzania katika Miradi Local Content.

“Mradi wa Reli ya kisasa ni moja ya miradi mikubwa sana hapa nchini na umeajili Watanzania wengi katika ngazi mbalimbali, mpaka mwezi Juni mradi huu umeajili watanzania 18,000 ambao ni sawa na 88% ya Wafanyakazi wote katika mradi na umeajiri makampuni ya Kitanzania takribani 640 ukilinganisha na makumuni 10 kutoka Nchi za nje” aliongezea Bi. Beng’i Issa

Kutokana na asili ya mradi huu umetumia bidhaa nyingi sana za Kitanzania mfano; kokoto, mchanga, simenti na nondo ambapo kampuni zipatazo 5 za uzalishaji wa nondo zimepata kazi katika mradi huu.

Mradi huu umepiga hatua nzuri ya kimaendeleo tangu kuanzishwa kwake mpaka mwezi Juni mradi umefikia 80%. Kutokea Dar es Salaam mpaka Ngerengere mradi umeisha kabisa na kuna maendeleo mazuri sana katika vituo vya Mkoani Morogoro na ujenzi unaendelea kuelekea mpaka Mkoani Dodoma.

.Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa mradi wa Standard Gauge Railway Bw. Ayoub Mdachi amesema kutakuwa na treni ya mizigo yenye urefu upatao kilomita 2 ambayo ni sawa na mabehewa 130. Treni hii itafanya safari zake kutoka Dar es Salaam na itapunguza kwa kiasi kikubwa adha ya usafiri Jijini Dar es Salaam.

Kwa kumalizia, Katibu Mtendaji ametoa wito kwa Kampuni za Kitanzania kujituma na kufanya kazi zao kwa weledi na umakini wa hali ya juu kwani hii itasaidia kuekeleza miradi hii kwa wakati na katika muda wa utekelezaji wa mradi uliopangwa.