Project Details

Imewekwa : 15-01-2019

Mradi wa Reli ya Kisasa

Project Description

Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa ni mfumo wa reli unaojengwa ambao unaunganisha Tanzania na nchi jirani za Rwanda, Uganda, Burundi, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Mahali Tanzania
  • Key Figures

  • Employees
    3526
  • Status
    Inayoanza

Mradi wa Ujenzi wa Reli ya kisasa

Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa ni mfumo wa reli unaojengwa ambao unaunganisha Tanzania na nchi jirani za Rwanda, Uganda, Burundi, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Malengo

Malengo ya mradi ni kupunguza gharama za usafiri, kupunguza muda wa kusafiri, ufikiaji rahisi kwa huduma mbalimbali za jamii kwa jumuiya ya eneo la mradi na uwezeshaji wa biashara kati ya Tanzania na nchi za jirani.

Njia hii ya reli yenye jumla ya 1,435 mm (4 ft 8 1/2 in) inalenga kurahisisha usafiri wa bidhaa kati ya bandari ya Dar es Salaam na miji ya Kigali, nchini Rwanda na baadaye Bujumbura, Burundi, na Goma, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kutoka bandari ya ziwa Victoria katika Jiji la Mwanza, feri zinatarajiwa kusafirisha bidhaa kati ya Mwanza na Port Bell na Port Bukasa, Kampala, mji mkuu wa Uganda. Reli hii ya SGR inatarajiwa kutumiwa na treni za abiria ambayo inatarajiwa kusafiri kilomita 160 (99 miili) kwa saa na treni za mizigo kusafiri kilomita 120 (75 mi) kwa saa.

Ujenzi wa Reli na Maeneo itakayopitia

Mradi ulianza mnamomwezi Aprili 2017 ambapo awamu ya kwanza, ujenzi ulianzia Dar es Salaam mpaka Morogoro kwa umbali wa Kilometa 300 (maili 186). Reli hiyo inaanzia katika bandari ya Bahari ya Hindi, Dar es Salaam hadi katika pwani ya Mwanza kwenye Ziwa Victoria ili kuunganisha nchi jirani.

Reli inapitia katika maeneo yafuatayo: Dar es Salaam, Morogoro, Makutopora (Dodoma), Tabora, Isaka (Shinyanga), Mwanza, Rusumo (Kigali,Rwanda), Bunjumbura (Burundi), Goma (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) na Kampala (Uganda).

Hatua za Ujenzi

Mfumo wa reli utakuwa na sehemu kadhaa kuu:

Sehemu ya Dar es Salaam - Morogoro

Sehemu hii ina kilomita 300 (186 mi), Ujenzi ulianza Aprili 2017 na mpaka hivi sasa umefikia asilimia 91.

Sehemu ya Morogoro-Dodoma

Kuanzia Morogoro kwenda Makutupora, mji mkuu Dodoma, una urefu wa kilomita 426 (265 mi) na mpaka sasa mradi huu umefikia asilimia 61.

Sehemu ya Dodoma-Isaka

Sehemu hii ina umbali wa kilomita 435 (270 mi), kutoka Makutupora, Dodoma, hadi Isaka, Tabora

Sehemu ya Isaka-Mwanza

Sehemu hii ina umbali wa takriban kilomita 220 (137 mi), inapitia jiji la Mwanza, kwenye mwambao wa kusini mwa Ziwa Victoria.

Sehemu ya Isaka-Rusumo

Hii ni sehemu ya Reli ya Kigali, ina umbali wa kilomita 371 (231 mi).

Fursa

Kuna nafasi za kazi kwa wahandisi, wafanyakazi wa kawaida na madereva na pia biashara kama vile za Mama Lishe, wafanyabiashara wadogowadogo (Marching Guys), bidhaa za viwandani n.k . Wahandisi na madereva wanapaswa kujiandikisha ili kupata fursa hizo pamoja na wafanyakazi wa kawaida wanapaswa kufikia eneo husika la mradi ili kupata fursa.

Hali ilivyo sasa

Hivi sasa, Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Reli ya kati kiwango cha kisasa ambayo inatoka Makutopora, Dodoma mpaka Tabora umefikia katika kiwango cha juu cha maandalizi. Utafiti umekamilika na Ujenzi kuanza hivi karibuni.

Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa hadi sasa umeshatoa Ajira kwa Watanzania 3,526 (Kati ya hizo, nafasi 2,328 ni Ujuzi wa Juu, nafasi 485 Ujuzi wa Kati na nafasi 713 Ujuzi wa Chini) dhidi ya Ajira 255 za Wageni (128 Ujuzi wa Juu na 127 Ujuzi wa Kati). Aidha, Mradi wa TIRP (Tanzania Inter Modal and Rail Development Project) ambao ni kama Sub Project ndani ya Mradi wa SGR umetoa Ajira 1,129 kwa Watanzania (233 Ujuzi wa Juu, 85 Ujuzi wa Kati na 811 Ujuzi wa Chini) dhidi ya Wageni 152 ambao wote wana Ujuzi wa Juu.