kilimo
Kilimo.
Kwa muda mrefu, nchi nyingi za Kiafrika zilikuwa zinategemea kilimo kuendeleza uchumi wao. 30% ya kipato cha nchi kinatoka kwenye kilimo wakati 60% za nafasi za kazi zinatoka sekta hii pia.
Kwa mujibu wa Tanzania Invest, mazao makuu yanayouzwa nje ni tumbaku, pamba, mkonge, korosho, kahawa, chai na karafuu. Malengo yamewekwa kwenye mazao haya na matokea yake ni kwamba uzalishaji umeongezeka kwa 44% kutoka 2008 – 2013. Kwa mujibu wa Tanzania Invest, tumbaku ni zao linaloingiza nchi pesa nyingi $318m kwenye mwaka 2015, ikifuatiwa na korosho $201m na kahawa $162m.
Pia kuna vikundi mbalimbali vya kilimo vilivyoundwa na serikali ili kuboresha usalama wa chakula na uzalishaji wa kilimo. SAGGOT – Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania na TADB – Tanazania Africulture Development Bank ni Baadhi ya Taasisi zinazosimamia vizuri upande wa kilimo.
Miradi mbalimbali za mikakati kilimo
- Kilimo cha Mpunga: hatua iliyofikiwa ni pamoja na: wakulima 820 kati ya wakulima 1,840 kupatiwa mafunzo juu matumizi ya mbegu bora na kuanzishwa kwa mashamba darasa 102; na jumla ya tani 10 za mbegu mama za mpunga zimezalishwa.
- Matumizi Bora ya Ardhi kwa Kilimo: hatua iliyofikiwa ni kuwezesha kupatikana kwa ardhi ya mashamba ya kilimo cha miwa ya Mkulazi (Morogoro Vijijini) lenye hekta 60,000, Bagamoyo hekta 10,000 na Mbigiri (Mvomero) ekari 12,000 ambayo yamekabidhiwa kwa wawekezaji; kuwezesha wananchi 400 wa kijiji cha Chanyumbu (Morogoro Vijijini) kupata hakimiliki za kimila; kuendelea na mradi wa matumizi endelevu ya ardhi katika lindimaji za mito Ruvu na Zigi; kutoa mafunzo kwa wakulima 8,800 juu ya kilimo cha makinga maji, upandaji wa miti na cha matuta katika kudhibiti mmomonyoko wa udongo.
- Hifadhi ya Chakula: hatua iliyofikiwa ni: ununuzi wa mahindi jumla ya tani 26,038.6 na kuongeza hifadhi ya mahindi kufikia tani 91,962.270 kutoka tani 65,923.67; na kuuza jumla ya tani 3,937.97 kwenye maeneo yaliyokuwa na upungufu wa chakula ikiwemo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Tathmini ya hali ya chakula nchini kwa mwaka 2017/18 imebainisha kuwa katika msimu wa kilimo wa 2016/2017, uzalishaji wa mazao ya chakula ulikuwa tani Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2018/19 30 15,900,864 za chakula ambapo tani 9,388,772 ni za mazao ya nafaka na tani 6,512,092 ni za mazao yasiyo nafaka. Mahitaji ya chakula kwa mwaka 2017/18 ni tani 13,300,034 ambapo tani 8,457,558 ni mazao ya nafaka na tani 4,842,476 ni mazao yasiyo nafaka, hiyo kutakuwa na ziada ya chakula kiasi cha tani 2,600,831.
- Mafunzo na Huduma za Ugani: hatua iliyofikiwa ni jumla ya wanafunzi 1,956 sawa na asilimia 88.9 ya lengo wamedahiliwa katika vyuo vya kilimo kwa ufadhili wa Serikali. Kati ya hao ngazi ya astashahada ni wanafunzi 1030 na stashahada ni 926 ambapo shilingi milioni 972 zimetumika. Jumla ya wakulima 15,230 wamepatiwa mafunzo ya matumizi sahihi ya viuatilifu vya zao la pamba katika Halmashauri za Bariadi, Itilima, Maswa na Meatu (Simiyu); Kwimba, Sengerema na Buchosa (Mwanza); Igunga na Nzega (Tabora); Chato na Geita (Geita); na Bunda, Musoma Vijijini na Serengeti (Mara). Vile vile, mafunzo ya kilimo shadidi cha mpunga (System for Rice Intensification – SRI) yametolewa kwa wataalam 48 kutoka katika skimu za umwagiliaji 17 zilizopo katika Halmashauri za Kilombero, Mvomero, Kilosa, Ulanga na Morogoro. Aidha, kupitia maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nane Nane) wadau mbalimbali wakiwemo wakulima wapatao 515,172 wamejifunza teknolojia mbalimbali za uzalishaji na usindikaji wa bidhaa na mazao ya kilimo.
- Tafiti za Kilimo: hatua ya utekelezaji iliyofikiwa ni ugunduzi wa aina 25 za mbegu mpya kwa mazao ya pamba (2), maharage (9), mahindi (3), karanga (3), njugumawe (2), tumbaku (5) na mpunga (1); kuzalisha mbegu mama zaidi ya tani 5.2 za pamba kilo 4,200 na mpunga kilo 1,050; na tani 98.9 za mbegu za awali za mazao ya pamba, viazi mviringo, mpunga, mahindi, ulezi, mtama, soya, na maharage; ugunduzi wa mbegu mpya za mazao mengine ikijumuisha miche 5,150 ya migomba, mihogo pingili 3,548,000 na vipandom 3,516,110 vya viazi vitamu; kushirikiana na COSTECH na CIMMYT kufanya utafiti wa ugunduzi wa mbegu za mahindi aina 6 zinazoonyesha kustahimili ugonjwa wa Maize Lethal Necrosis Disease (MLND); na kuchora ramani za mtawanyiko wa magonjwa ya mazao nchini.
- Skimu za Umwagiliaji Mpunga: hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa usanifu wa kina na kuanza kwa mchakato wa kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa maghala 5 katika skimu za Msolwa - Ujamaa na Njage (Kilombero), Kigugu na Mbogo (Mvomero) na skimu ya Mvumi (Kilosa); kusainiwa kwa mikataba minne (4) kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa maeneo yatakayojengwa miundombinu ya umwagiliaji kwa skimu za Lwanyo (Mbarali), Ibanda (Sengerema), Luiche (Kigoma) na Gidahababieg (Hanang); na kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu kwa skimu 5 za Msolwa - Ujamaa na Njage (Kilombero); Kigugu na Mbogo (Mvomero ) na skimu ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2018/19 31 Mvumi (Kilosa).
- Mafanikio mengine katika Sekta ya Kilimo ni pamoja na:
- Uzalishaji wa mazao ya jamii kunde unakadiriwa kufikia tani 2,317,807;
- Kuzalishwa na kusambazwa kwa tani 11,500 za mbegu mpya za Pamba na ununuzi wa viuatilifu chupa 5,750,000;
- Kuzalishwa na kusambazwa kwa miche 1,163,758 ya kahawa;
- Kuanza ujenzi wa vihenge vya kisasa (silos) vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 25,000 za mahindi ambavyo vitaongeza uwezo wa Wakala wa Hifadhi ya Chakula kuhifadhi tani 501,000 za nafaka;
- Kukamilika kwa ujenzi wa skimu ya kisasa ya umwagiliaji Dakawa - Morogoro yenye jumla ya hekta 2,000; ujenzi wa barabara za mashambani kilomita 35 ambao umekamilika kwa asilimia 80 na ufungaji wa pampu za skimu unaendelea katika skimu ya Dakawa;
- Ujenzi wa skimu ya umwagiliaji Mafuruto - Iringa vijijini kukamilika kwa asilimia 90;
- Kuwezesha ununuzi wa pamoja wa mbolea tani 54,000 hivyo kuongeza kiasi cha mbolea kilichoingizwa nchini kufikia tani 229,839 ambazo zimesambazwa katika maeneo mbalimbali nchini;
- Kuandaliwa kwa Mkakati wa Kitaifa wa Usimamizi wa Mazao baada ya Mavuno wenye lengo la kupunguza upotevu wa mazao ya chakula katika mnyororo wa uzalishaji; na
- Kuongezeka kwa uzalishaji wa korosho kutoka tani 265,237 mwaka 2016/17 hadi kufikia tani 294,568.
Mifugo
- Kuimarisha Uzalishaji katika Sekta ya Mifugo Hatua iliyofikiwa ni:
- kuzalishwa kwa mitamba 590 kutoka katika mashamba ya Serikali na NARCO;
- kuanzishwa kwa vituo 154 vya kukusanyia maziwa kwenye maeneo yenye mfumo wa masoko unaounganisha viwanda vya kusindika maziwa;
- ikuimarisha kituo cha uhamilishaji cha NAIC – Usa River kwa ununuzi wa madume bora 11;
- kukarabatiwa kwa maabara na kununua vifaa vya maabara (bailer, mtungi wa lita 2,000 wa kusafirishia kimiminika baridi cha nitrejeni, na mitungi 5 ya lita 50 kila moja ya kuhifadhia mbegu pamoja na kimiminika cha nitrojenji);
- kupatiwa mafunzo ya uhimilishaji kwa wataalam na wasimamizi wa vituo 9 vya uhimilishaji;
- kukarabatiwa kwa mnada wa Kirumi;
- kukamilika kwa mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa vijiji 1,695; na
- kutengwa kwa hekta milioni 2.545 kwa ajili ya ufugaji katika vijiji 741 vilivyoko katika mikoa 22 zimepatikana na kusambazwa. Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2018/19 32
- Magonjwa ya Milipuko na Magonjwa ya Tahadhari Lengo la kuzalisha chanjo za mifugo limetekelezwa ambapo: Jumla ya chanjo dozi 16,107,900 za mdondo (I2), dozi 341,700 za kimeta, dozi 128,600 za chambavu na dozi 10,000 za brucellosis zimezalishwa; ng‟ombe 70,260 wamepatiwa chanjo za ndigana kali na dawa za kuogesha mifugo; na dozi 1,020,000 za chanjo ya ugonjwa wa homa ya Mapafu ya ng‟ombe (CBPP).
- Uwekezaji wa tija katika Ranchi za Taifa (NARCO) Kazi zilizofanyika ni: ununuzi wa ng‟ombe 1,175 kutoka kwa wafugaji wa asili kwa ajili ya kuendeleza programu ya unenepeshaji; kuchinja ng‟ombe 2,488 walionenepeshwa; kutoa ushauri wa ufugaji bora kwa wawekezaji katika ranchi ndogo waliowekeza jumla ya ng‟ombe 87,601, mbuzi 12,432 na kondoo 9,537.
- Vituo vya Utafiti, Ugani wa Mifugo na Mafunzo Hatua iliyofikiwa ni: kusambazwa kwa teknolojia 27 za utafiti uliofanywa na TALIRI katika wilaya 41 nchini ambapo vijiji 135 vyenye jumla ya kaya 3,676 zilihusishwa; wafugaji 21500 na ng‟ombe 7,401,661 wametambuliwa na ng‟ombe 32,730 wamesajiliwa na kuwekewa alama (ear tag); na kutolewa kwa mafunzo ya utunzaji wa mifugo kwa wadau 1,991 katika mikoa ya Arusha, Manyara, Morogoro, Dodoma, Pwani, Mwanza, Kagera, Kilimanjaro, Mara, Iringa, Mbeya, Njombe, Rukwa, Songwe, Shinyanga, Singida na Tanga; na kudahiliwa kwa Wanafunzi 2,137 kati ya lengo la wanafunzi 2,600 katika ngazi ya cheti na diploma katika mwaka wa masomo 2017/18.
- Miundombinu ya Maji ya Mifugo Hatua iliyofikiwa ni: ujenzi wa mabwawa 2 ya Olyapasei (Kiteto) na Kwamaligwa (Kilindi), na lambo la Masusu (Ngorongoro). Ujenzi wa miundombinu hii inafanya jumla ya miundombinu iliyojengwa na kukarabatiwa kuwa mabwawa matatu (3), malambo 1,378, visima virefu 101, minada ya upili 12, minada ya mipakani 11 na minada ya awali 445.
- Maeneo ya Malisho Hatua iliyofikiwa ni: kutengwa kwa hekta 10,378.53 za ardhi kwa ajili ya maeneo ya ufugaji kwenye vijiji 13 katika wilaya za Makete, Kilolo, Tanganyika, Mpanda na Kalambo; kuzalishwa kwa marobota 1,141,946 ya malisho kutoka kwenye mashamba ya Serikali na sekta binafsi; kufanyika kwa ukaguzi wa maeneo 72 ya kuzalisha, kuhifadhi na kukuza vyakula vya mifugo; kusajiliwa kwa viwanda 26 vya kutengeneza vyakula vya mifugo na maeneo matano (5) ya kuhifadhia na kuuza vyakula hivyo; na kutoa mafunzo kwa wakaguzi tisa (9) na watengenezaji 10 wa vyakula vya mifugo ili kuwajengea uwezo. Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2018/19 33
- Mfumo wa Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Mifugo Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea kutekelezwa kwa zoezi la utambuzi kwa njia ya chapa ya moto kwa mifugo ya ng‟ombe na punda katika halmashauri zote nchini, ambapo hadi kufikia mwezi Aprili, 2018 jumla ya ng‟ombe 17,045,944 wamepigwa chapa ikiwa ni asilimia 98.0 ya lengo la kupiga chapa ng‟ombe 17,390,090. Vile vile, jumla ya ng‟ombe wa maziwa 58,214 wamevishwa hereni ambayo ni asilimia 7.4 ya lengo la kuvisha ng‟ombe wa maziwa 782,995. Punda 57,797 wamepigwa chapa ikiwa ni asilimia 10.1 ya lengo la kupiga chapa punda 572,357. Mfumo huu utaimarisha usimamizi wa mifugo na kuchangia kwa kiasi kikubwa kumaliza migogoro kwa wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.
Uvuvi
- Kuimarisha na Kuendeleza Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi Hatua iliyofikiwa: Kuboreshwa kwa mfumo wa ukusanyaji Takwimu za meli na uvuvi wa samaki kwa kuanzisha Kanzidata; kuendelea kukusanya takwimu za uvuvi wa samaki aina ya Jodari na jamii zake unaofanyika katika Eneo la Ukanda wa Kiuchumi wa bahari; kuimarisha hifadhi ya bahari na maeneo tengefu kwa kutumia kamera zinazoweza kupiga picha ndani ya maji, maturubai viona mbali (binoculars), Radio Calls na GPS kupitia mradi wa usimamizi Shrikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish); kuongezeka kwa doria za anga na baharini kupitia programu ya IOC-SMARTFish na Mradi wa SWIOFish kwa kutumia ndege; kuendelea na taratibu za kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) ambapo kufikia Julai 2018, shirika litanza kufanya kazi na kuwezesha nchi yetu kuwa na meli za kitaifa (National Fleet) kwa ajili ya uvuvi wa Bahari Kuu ili kuongeza mchango wa Sekta ya Uvuvi katika pato la Taifa; na kuongezeka kwa uvunaji wa samaki kutoka tani 362,595 mwaka 2016 hadi tani 387,543 mwaka 2017 wenye thamani ya shilingi trilioni 1.74.
- Ukuzaji viumbe kwenye maji Hatua iliyofikiwa: Kuimarisha na kuendeleza vituo vitano (5) vya ufugaji samaki wa maji baridi vya Ruhila (Songea), Mwamapuli (Tabora), Kingolwira (Morogoro), Nyegedi (Lindi) na Nyamirembe (Chato) kwa ajili ya kuzalisha vifaranga; kuzalishwa kwa vifaranga vya samaki na kambamiti 15,119,757 katika vituo vya Serikali vya Ruhila na Kingolwila na vifaranga 14,924,569 katika sekta binafsi; kuimarishwa kwa vituo viwili (2) vya maji bahari vya Machui (Tanga) na Mbegani (Pwani) kwa ajili ya kuzalisha vifaranga milioni tatu kwa kufunga mfumo wa maji baridi katika jengo la kituo cha Mbegani baridi katika jengo. Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2018/19.
- Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi wa Bahari Hatua iliyofikiwa: kukamilika kwa taratibu za manunuzi za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi ambapo Kampuni ya Sering Ingegneria ya Italy kwa kushirikiana na Kampuni ya Kitanzania inayoitwa Doch Tanzania Limited zimekamilisha hatua za awali za kufanya kazi hii.