viwandaa
Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, imeweka mikakati ya kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati ambao pamoja na mambo mengine, una lengo la kuifanya nchi kuwa ya viwanda.
Katika kuhakikisha azma hii inatimia, Serikali imeandaa mpango wa miaka mitano wa maendeleo ya Taifa ambao pamoja na mengine unasisitiza ujenzi wa viwanda ambavyo vitachangia ukuaji wa uchumi na kutatua changamoto za ukosefu wa ajira.
Wadau mbalimbali wameitikia azma hii ya Serikali na hivyo miradi mbalimbali ya ama kuanzisha viwanda au kufufua viwanda inaendelea Tanzania nzima.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono mafundi wa Kiwanda cha Victoria molders and polybags mara baada ya kutengeneza Tanki la kuhifadhia maji.
Vifuatavyo ni baadhi ya Viwanda vilizinduliwa na Mhe Rais kati ya mwaka 2017 na 2019
- kiwanda cha Global Packing kilichopo Kibaha mkoani Pwani
- Viwanda vya mradi wa upanuzi wa mtambo wa maji wa Ruvu Juu na uzalishaji wa mabomba,
- Mradi wa Upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji Ruvu juu Mlandizi Mkaoni Pwani
- mkubwa wa kusafisha na kuzalisha Maji kwa miji ya Pwani na Dar es Salaam.
- kiwanda cha Global Packing kilichopo Kibaha mkoani.kiwanda cha kutengeneza matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
- .kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi mkoani Pwani.
- viwanda vya chaki na kiwanda cha usindikaji maziwa Simiyu
- Kiwanda cha kuchakacha mahindi Mlale – Ruvuma
- Kiwanda cha kusaga nafaka cha MeTL – Kurasini Dar Es Salaam
- Kiwanda cha Sayona – Mwanza
- Kiwanda cha Victoria Molders and polybags – Mwanza
- Kiwanda cha Prince Pharmaceuticals – mwanza
- Kiwanda cha Chai cha UNILEAVER Kabambe – Njombe
- Kiwanda cha Superdoll – Vingunguti Dar er Salaam
- Kiwanda cha Sigara cha Philips Moris International – Morogoro
Ushirikishwaji wananchi
Viwanda vina uhusiano wa karibu na miundo mbinu, mawasiliano na kilimo. Hivyo kama nchi itakuwa na viwanda pia sekta hizi zitaimarika.
- Nafasi za ajira za juu, kati na chini
- Wakulima kuchamgamkia malighafi zitakazo hitajika viwandani
- Wakala wa bidhaa za viwandani
- Mafundi wa aina zote, ujenzi, mitambo, n.k.
- Kupata teknolojia mpya
- Kuisaidia nchi kukua kiuchumi,
- kupata fedha za kigeni,
Serikali inahakikisha kuwa uchumi wa Nchi yetu unakua kwa kuifanya Tanzania kuwa Nchi ya viwanda. Katika kujenga uchumi wa viwanda, Serikali imehamasisha wawekezaji wa ndani na nje kujenga viwanda vidogo, vya kati na vikubwa. Viwanda vinavyopewa kipaumbele ni vile vinavyotumia malighafi zinazopatikana hapa nchini, vinavyotoa ajira kwa watu wengi na vinavyozalisha bidhaa zenye soko hapa ndani na nje ya Nchi.
Tumeona mwitikio mkubwa wa sekta binafsi kuwekeza katika viwanda. Baadhi ya viwanda vilivyoanzishwa katika kipindi cha kuanzia Novemba, 2015 ni pamoja na; kiwanda cha kusindika maziwa cha Milkcom Ltd kilichopo Kigamboni – Dar-es-Salaam ambacho uwekezaji wake ni Shilingi Bilioni 44 na kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 67.5 za maziwa kwa mwaka na kutoa ajira kwa watu 500; kiwanda cha nyama cha Meat King Ltd kilichopo eneo la Moshono- Mkoa wa Arusha kimewekeza Shilingi Bilioni 5.5 kwa ajili ya kusindika nyama ya ng’ombe, kuku na kondoo; kiwanda cha Lakairo Polybag kilichopo Mwanza ambacho uwekezaji wake ni Shilingi Bilioni 4 chenye uwezo wa kuzalisha magunia ya sandarusi milioni 10 kwa mwaka; kiwanda cha Global Packaging kilichopo Kibaha – Pwani kimewekeza Shilingi Bilioni 8 chenye uwezo wa kuzalisha magunia ya sandarusi milioni 11.75 kwa mwaka na ajira ya watu 110. Kiwanda cha Nyama kilichopo hapa Dodoma kinachinja Ng’ombe 350 – 500 kwa siku.
Baadhi ya viwanda vikubwa vinavyoendelea kujengwa hapa nchini ni: Kilua Steel Group– kiwanda cha nondo kinazalisha tani 2000 kwa siku; kiwanda cha marumaru cha Goodwill kilichopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani; kiwanda cha kusokota nyuzi za pamba cha NAMERA kilichopo Gongolamboto, Dar-es-Salaam; kiwanda cha kukausha mbogamboga cha Vegeta Padravka Ltd kilichopo Bagamoyo -Pwani ambacho uwekezaji wake unatarajiwa kuwa Shilingi Bilioni 9.9 na kiwanda cha kusindika nyama cha Nguru Hills Ranchkinachojengwa Mvomero – Morogoro ambacho kitahitaji ng’ombe 50,000 na mbuzi 60,000 kwa mwaka.
Serikali inaweka mkazo wa ujenzi wa viwanda, kila Mkoa ili kuzalisha bidhaa pia kupunguza tatizo la ajira nchini.
Sehemu ya hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kuwasilisha taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi mwaka 2015-2020 katika kipindi cha Novemba 2015 hadi Novemba 2017 katika mkutano mkuu wa CCM unaofanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma, kuanzia tarehe 18- 19 Desemba 2017.
Baadhi ya Miradi ya Viwanda
- Uendelezaji wa Viwanda Vidogo – SIDO: Hatua iliyofikiwa ni:
- i.Kukamilika kwa michoro kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za kutoa huduma na kuongeza maeneo ya kufanyia kazi wajasiriamali katika mikoa ya Simiyu, Katavi na Geita na kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa ofisi hizo;
- ii.Ujenzi wa majengo ya kufanyia shughuli za viwanda kwa wajasiriamali wadogo (industrial sheds) katika mikoa ya Geita, Kagera, Mtwara, Njombe, Dodoma, Simiyu na Manyara unaendelea;
- iii.Kuwezesha uanzishwaji wa viwanda vipya vidogo vya aina mbalimbali 429 na kuzalisha ajira mpya 1,287; na
- Kuhamasisha wajasiriamali 520 kushiriki katika ujenzi wa viwanda
- Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini (CAMARTEC): kazi zilizotekelezwa ni:
- kuendelea kubuni teknolojia na kutengeneza zana mbalimbali; kutumia matokeo ya utafiti wa mwaka 2016/17 kuhusu mahitaji ya zana za kilimo nchini na kuanza kushirikiana na wajasiriamali wa ndani kuendeleza ubunifu wao na kutengeneza zana za kilimo;
- Kubuni na kutengeneza mashine 64 za kupandia mbegu za pamba, kusaga karanga, kukausha mbogamboga na kukata majani; ujenzi wa mitambo 55 ya biogesi pamoja na kutoa mafunzo na elimu ya utumiaji wa biogesi; na
- Kukamilika kwa tafiti tatu zinazohusiana na matumizi ya nishati mbadala ya biogesi.
Aidha, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2018/19 kituo kimeandaa Kanuni za Majaribio ya Zana za Kilimo ambazo zimechapishwa kwenye Gazeti la Serikali Tarehe 23 Februari 2018. Hatua hiyo itasaidia kujenga uelewa na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kufanyia majaribio zana za kilimo.
- Ujenzi na Ukarabati wa Viwanda vya Kuchakata Ngozi:
- Ukarabati wa majengo ya kiwanda cha ngozi na bidhaa za ngozi cha Karanga-Moshi unaendelea;
- Zabuni kwa ajili ya ununuzi wa mitambo mipya itakayowezesha kiwanda kuzalisha jozi 400 za viatu kwa siku zipo katika hatua za mwisho; na
- Eneo la ujenzi wa kiwanda kipya kitakachokuwa na uwezo wa kuchakata ngozi futi za mraba milioni 3.75 na kutengeneza jozi 4,000 za viatu kwa siku pamoja na bidhaa nyingine zinazotokana na ngozi limepatikana. Tafiti mbalimbali ikiwemo Geotechnical & Topographical surveys, Environmental Impact and Social Assesment – EIA zimefanyika na michoro ya majengo imeandaliwa.
- Mradi wa Magadi Soda – Bonde la Engaruka, Arusha: Hatua iliyofikiwa ni
- Kukamilika kwa zoezi la upimaji wa ardhi ya eneo la mradi na uthamini wa wa mali za wananchi ili kujua kiasi cha fidia kitakachohitajika;
- Michoro ya matumizi ya matumizi ya ardhi iko hatua za mwisho kukamilishwa. Kampuni ya Hi-Tech ya Misri imeonesha nia kuwekeza na makubaliano ya mwanzo – MOU kati yake na NDC yamefanyika.
- Mradi wa Kuunganisha Matrekta TAMCO-Kibaha: hatua iliyofikiwa ni
- Kuunganishwa kwa jumla ya kuwasili nchini kwa Semi Knocked Down (SKD) za matrekta 727 kati ya matrekta 2,400 yaliyoainishwa katika mkataba kwa ajili ya kiwanda;
- Matrekta 148 na majembe (disc plough) 94 na kuhakikiwa ubora wake na CAMARTEC kabla ya kuuzwa kwa wakulima;
- Ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha matrekta unaendelea na unategemea kukamilika mwezi Juni, 2018.
- Kiwanda cha Kutengeneza Matairi Arusha: hatua iliyofikiwa ni
- kukamilika kwa utafiti wa namna bora ya kufufua kiwanda kwa kuangalia mitambo iliyopo, teknolojia na uwezekano wa uwekezaji kutekelezwa na sekta binafsi. Utafiti unapendekeza Sekta binafsi kushiriki katika uwekezaji wa kiwanda hicho. Mpaka sasa, kamati maalum ya serikali inaendelea kupitia mpango wa kiwanda hicho ili kuamua utaratibu utakaofaa katika uwekezaji kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.
- Shirika la utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO): kazi zilizotekelezwa ni:
- Kuendelea kuimarisha maabara kwa kuhakiki maabara za makaa ya mawe ili kufikia viwango vya kimataifa;
- iKuendelea na jitihada za uanzishwaji na uhakiki wa maabara ya mafuta na gesi;
- Kuwasilishwa kwa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2018/19 29 maombi ya usajili wa maabara ya mazingira kwa mamlaka ya Uhakiki (SADCAS), kuendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kununua vifaa na uhakiki wa maabara ya vifaa vya ujenzi;Kuandaa na kuwasilisha kwa wafadhili andiko kwa ajili ya kutafuta fedha za kuanzisha maabara ya vipimo vya chuma kigumu (iron and steel);
- Kutoa huduma za kitaalam viwandani; na
- Kutoa huduma za upimaji wa uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za uzalishaji viwandani na kutoa ushauri.
- Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo (TEMDO): kazi zilizofanyika ni:
- Maboresho ya karakana ya taasisi kwa kupata na kusimika mashine mpya tano;
- Kukamilika kwa usanifu, uendelezaji na utengenezaji wa mashine tatu za kuchakata bidhaa za marumaru;
- Kutembelea na kushauriana na wadau mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya teknolojia zilizobuniwa kwa ajili ya uzalishaji wa mafuta yatokanayo na mbegu za alizeti;
- Kukamilika kwa utengenezaji wa chasili cha mtambo wa uzalishaji umeme kutokana na nguvu za maji uitwao crossflow Turbine na usanifu wa mtambo wa kuzalisha umeme unaotokana na nguvu za maji uitwao Reverse Pump Turbine;
- Kukusanywa kwa taarifa muhimu za makaa ya mawe yanayopatikana nchini na teknolojia zitakazotumia kutengeneza brikwiti za makaa ya mawe (coal dust briquettes) zitakazotumika kupikia.