Railways
MRADI WA UJENZI WA RELI YA KISASA (STANDARD GAUGE RAILWAY)
Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa ni mfumo wa reli unaojengwa ambao unaunganisha Tanzania na nchi jirani za Rwanda, Uganda, Burundi, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Malengo
Malengo ya mradi ni kupunguza gharama za usafiri, kupunguza muda wa kusafiri, ufikiaji rahisi kwa huduma mbalimbali za jamii kwa jumuiya ya eneo la mradi na uwezeshaji wa biashara kati ya Tanzania na nchi za jirani.
Njia hii ya reli yenye jumla ya 1,435 (4 ft 8 1/2 in) inalenga kurahisisha usafiri wa bidhaa kati ya bandari ya Dar es Salaam na miji ya Kigali, nchini Rwanda na baadaye Bujumbura, Burundi, na Goma, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kutoka bandari ya ziwa Victoria katika Jiji la Mwanza, feri zinatarajiwa kusafirisha bidhaa kati ya Mwanza na Port Bell na Port Bukasa, Kampala, mji mkuu wa Uganda. Reli hii ya SGR inatarajiwa kutumiwa na treni za abiria ambayo inatarajiwa kusafiri kilomita 160 (99 miili) kwa saa na treni za mizigo kusafiri kilomita 120 (75 mi) kwa saa.
Ujenzi wa Reli na Maeneo itakayopitia
Mradi ulianza mnamo mwezi Aprili 2017 ambapo awamu ya kwanza, ujenzi ulianzia Dar es Salaam mpaka Morogoro kwa umbali wa Kilometa 300 (maili 186). Reli hiyo inaanzia katika bandari ya Bahari ya Hindi, Dar es Salaam hadi katika pwani ya Mwanza kwenye Ziwa Victoria ili kuunganisha nchi jirani.
Reli inapitia katika maeneo yafuatayo: Dar es Salaam, Morogoro, Makutopora (Dodoma), Tabora, Isaka (Shinyanga), Mwanza, Rusumo (Kigali,Rwanda), Bujumbura (Burundi), Goma (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) na Kampala (Uganda).
Hatua za Ujenzi
Mfumo wa reli una sehemu kadhaa kuu:
Sehemu ya Dar es Salaam - Morogoro
Sehemu hii ina kilomita 300 (186 mi), Ujenzi ulianza Aprili 2017, na unaendelea kwa kujenga nguzo pamoja na kuweka mataluma.
Sehemu ya Morogoro-Dodoma.
Kuanzia Morogoro kwenda Makutupora, mji mkuu Dodoma, una urefu wa kilomita 426 (265 mi).
Sehemu ya Dodoma-Isaka
Sehemu hii ina umbali wa kilomita 435 (270 mi), kutoka Makutupora, Dodoma, hadi Isaka, Tabora
Sehemu ya Isaka-Mwanza
Sehemu hii ina umbali wa takriban kilomita 220 (137 mi), inapitia jiji la Mwanza, kwenye mwambao wa kusini mwa Ziwa Victoria.
Sehemu ya Isaka-Rusumo
Hii ni sehemu ya Reli ya Kigali, ina umbali wa kilomita 371 (231 mi).
Fursa
Kuna nafasi za kazi kwa wahandisi, wafanyakazi wa kawaida na madereva na pia biashara kama vile za Mama Lishe, wafanyabiashara wadogowadogo (Marching Guys), bidhaa za viwandani n.k . Wahandisi na madereva wanapaswa kujiandikisha ili kupata fursa hizo pamoja na wafanyakazi wa kawaida wanapaswa kufikia eneo husika la mradi ili kupata fursa.
Hali ilivyo sasa
Hivi sasa, Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Reli ya kati kiwango cha kisasa ambayo inatoka Makutopora, Dodoma mpaka Tabora umefikia katika kiwango cha juu cha maandalizi. Utafiti umekamilika na Ujenzi kuanza hivi karibuni.
Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa hadi sasa umeshatoa Ajira kwa Watanzania 14000 (Kati ya hizo, nafasi ni Ujuzi wa Juu, nafasi Ujuzi wa Kati na nafasi 127 Ujuzi wa Chini) dhidi ya Ajira za Wageni ( 128 Ujuzi wa Juu na Ujuzi wa Kati). Aidha, Mradi wa TIRP (Tanzania Inter Modal and Rail Development Project) ambao ni kama Sub Project ndani ya Mradi wa SGR umetoa Ajira kwa Watanzania (233 Ujuzi wa Juu, 85 Ujuzi wa Kati na 811 Ujuzi wa Chini) dhidi ya Wageni 152 ambao wote wana Ujuzi wa Juu.
- Unaweza pia kupata habari zaidi hapa: http://www.rahco.go.tz