Reli
MRADI WA UJENZI WA RELI YA KISASA (STANDARD GAUGE RAILWAY)
Kuanzia Morogoro kwenda Makutupora, mji mkuu Dodoma, una urefu wa kilomita 426 (265 mi).
Sehemu ya Dodoma-Isaka
Sehemu hii ina umbali wa kilomita 435 (270 mi), kutoka Makutupora, Dodoma, hadi Isaka, Tabora
Sehemu ya Isaka-Mwanza
Sehemu hii ina umbali wa takriban kilomita 220 (137 mi), inapitia jiji la Mwanza, kwenye mwambao wa kusini mwa Ziwa Victoria.
Sehemu ya Isaka-Rusumo
Hii ni sehemu ya Reli ya Kigali, ina umbali wa kilomita 371 (231 mi).
Fursa
Kuna nafasi za kazi kwa wahandisi, wafanyakazi wa kawaida na madereva na pia biashara kama vile za Mama Lishe, wafanyabiashara wadogowadogo (Marching Guys), bidhaa za viwandani n.k . Wahandisi na madereva wanapaswa kujiandikisha ili kupata fursa hizo pamoja na wafanyakazi wa kawaida wanapaswa kufikia eneo husika la mradi ili kupata fursa.
Hali ilivyo sasa
Hivi sasa, Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Reli ya kati kiwango cha kisasa ambayo inatoka Makutopora, Dodoma mpaka Tabora umefikia katika kiwango cha juu cha maandalizi. Utafiti umekamilika na Ujenzi kuanza hivi karibuni.
Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa hadi sasa umeshatoa Ajira kwa Watanzania 14000 (Kati ya hizo, nafasi ni Ujuzi wa Juu, nafasi Ujuzi wa Kati na nafasi 127 Ujuzi wa Chini) dhidi ya Ajira za Wageni ( 128 Ujuzi wa Juu na Ujuzi wa Kati). Aidha, Mradi wa TIRP (Tanzania Inter Modal and Rail Development Project) ambao ni kama Sub Project ndani ya Mradi wa SGR umetoa Ajira kwa Watanzania (233 Ujuzi wa Juu, 85 Ujuzi wa Kati na 811 Ujuzi wa Chini) dhidi ya Wageni 152 ambao wote wana Ujuzi wa Juu.
- Unaweza pia kupata habari zaidi hapa: http://www.rahco.go.tz