Usafiri wa Anga
Ndege mpya aina ya Bombardier Q-400 iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania imetua uwanja wa Mwanza na kupokelewa na wananchi na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais John Magufuli.
Kuwasili kwa ndege hiyo kunafanya idadi ya ndege mpya zilizonunuliwa na Serikali katika jitihada za kulifufua Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) kufikia 8.
Tangu iingie madarakani Serikali ya awamu ya tano, 2015 inatekeleza Mradi wa kufufua ATCL ambapo imepanga kununua ndege mpya 11 za aina na ukubwa tofauti.
Ndege zilizopo kwa sasa ni:
1. Ndege 2 aina ya Boeing 787-8 Dreamliner
2. Ndege 2 aina ya Airbus 220-300
3. Ndege 4 aina ya Bombardier Dash 8-400/300
Ndege zingine tatu zilizosalia zinatarajiwa kuwasili nchini kwa nyakati tofauti mwaka 2020.